GET /api/v0.1/hansard/entries/641757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641757/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia Mswada huu wa ardhi wa 2015. Ningependa kusema kuwa ninapinga Mswada huu vikali kwa sababu unakiuka Katiba ya Kenya. Kuna Mbunge aliyesimama na kutukosoa Wabunge ambao tunapinga Mswada huu. Alisema kuwa Tume ya Ardhi haiwezi kufanya kazi pekee na ni lazima ifanye kazi na Wizara ya Ardhi. Ningependa kumkumbusha Mbunge huyo kuwa Kipengele cha 249(2)(b) cha Katiba kinasema kuwa: “Tume ya Ardhi ni huru kufanya kazi zake bila kuelekezwa kazi na mtu au shirika lolote lile.”"
}