GET /api/v0.1/hansard/entries/641758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641758/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Maandiko ya kukumbusha habari katika Mswada huu yanasema kuwa sheria hii inataka kupunguza nguvu za Tume ya Ardhi ili ishughulikie tu masuala ya ardhi za umma lakini Kipengele cha 67(2)(c) cha Katiba kinasema kuwa: “Tume ya Ardhi inapaswa kushauri Serikali kuu kuhusu uandikishaji wa ardhi zote katika nchi yetu.” Katika mambo hayo mawili, sheria hii imekiuka Katiba. Zaidi ya hapo, inapunguza nguvu za Tume ya Ardhi kutengeneza sera za masuala ya ardhi. Kipengele cha 67(2)(b) cha Katiba kimeipa Tume ya Ardhi hii nguvu lakini Mswada huu unaiondoa. Vilevile, Mswada huu unataka kupunguza nguvu za Tume katika kuamua jinsi ardhi za umma zinagawanywa. Imekiuka Katiba katika sehemu nyingi sana. Ningeomba wale waliotunga Mswada huu waurejelee na wauandike jinsi unavyotakikana. Wasiseme kwamba tuna muda mfupi wa kuandika sheria kama kisingizio cha kuleta sheria ambayo haitafaa."
}