GET /api/v0.1/hansard/entries/641760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641760,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641760/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Masuala ya dhuluma za kihistoria yamezungumziwa kwa ufupi sana na yanafaa yazungumziwe kwa kinaga ubaga ili tuangalie njia ambazo watu wamekuwa wakidhulumiwa kwa sababu ya ardhi hizo siku zilizopita. Sababu kubwa ya kuleta Katiba hapa nchini na kuibadilisha ilikuwa kuhakikisha kuwa shida zote ambazo tumekuwa nazo kama nchi pamoja na shida za ardhi zimetafutiwa suluhu. Sheria hii inaturejesha pale tulipokuwa kabla ya kupata Katiba - siku za giza na kudhulumiana."
}