GET /api/v0.1/hansard/entries/641761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 641761,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641761/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Sheria za kufurushwa kwenye ardhi hazijazungumziwa licha ya kuwa wamesema kuwa zitazungumziwa. Hivi sasa, katika maeneo ya Mombasa, Changamwe na Kisauni, kuna watu wameahidiwa kuwa wataondolewa Ijumaa katika ardhi yao. Wizara ya Ardhi inafanya hivi na vipi inaweza kufanya hivyo bila sheria ya kusema jinsi watu wanavyotakikana kuhamishwa? Tunapinga jambo hilo na mambo ya kuhamisha lazima iwe katika sheria kama hii. Waziri wa Ardhi amepewa majukumu ya Tume ya Ardhi. Kwa mfano, masuala ya kuamua ardhi ni ya mtu fulani. Sheria hii inasema kuwa makamishna wa Tume ya Ardhi wataandikwa kazi na Tume ya Kuwaajiri Wahudumu wa Umma. Hicho ni kinyume cha Katiba. Katiba inasema kuwa makamishna watateuliwa na Rais na majina yao kuletwa Bungeni ndio wapitishwe au wakataliwe. Makamishna wamechukuliwa kama viongozi wa bodi ambayo Serikali inaajiri. Tume ya Ardhi ni huru kama vile nilivyosema awali. Sheria hii imeondoa bodi za kaunti za kusimamia masuala ya ardhi. Katiba imepeana kazi kwa serikali ya kaunti kama njia ya kukabiliana na masuala ya ardhi kupitia bodi hii. Tumeondoa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}