GET /api/v0.1/hansard/entries/641763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 641763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641763/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Zile njia ambazo watu wanaweza kukaa na kukubaliana kuhusiana mizozo ya ardhi zimeondolewa; kwamba si lazima kuenda kortini kuzungumzia shida zao. Imezidi kutia mwananchi katika dhiki na shida. Katika Mkoa wa Pwani, kuna asilimia zaidi ya 60 ya watu ambao wako kwenye ardhi ambazo hazijasajiliwa. Umaskini ambao uko katika nchi hii hususan Mkoa wa Pwani ni mkubwa ilhali unamwambia mtu azidi kugharamika kwa sababu ya kutetea haki yake ya kuishi pahali ambapo ni kwao tangu jadi na ambapo vizazi vyote vya familia vimetoka. Kitu cha mwisho ambacho ninataka kusema ni kuwa hatutakubali kamwe kurejeshwa nyuma katika nchi hii. Sio kwa masuala ya ardhi pekee bali katika masuala yote ambayo wananchi wenyewe wa Kenya wameamua kuwa tusonge mbele na wakapitisha Katiba. Tunapata watu wawili au watatu wanatuletea sheria ambayo itaturejesha kwenye siku za giza na itaendelea kuwadhulumu Wakenya kama vile walivyokuwa wakidhulumiwa hapo awali. Wanatuletea sheria ambayo haileti marekebisho au mabadiliko yoyote. Kwa hayo machache, ninapinga sheria hii."
}