GET /api/v0.1/hansard/entries/641837/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641837,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641837/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "s",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nikiangalia sehemu ambayo natoka ya Taita, ardhi imenyakuliwa na kuchukuliwa. Unapata Wataita wanakaa kwa theruthi moja tuu ya ardhi yao. Hiyo nyingine yote imeenda. Ndiyo maana tulikuwa tunatarajia kwamba tutapata nafasi ya kipekee ya kuleta sheria ambazo zitangalia wale watu walio dhulumiwa na mambo ya ardhi. Kwa sababu ya hekima ambayo hii Kamati iko nayo, ilionelea ni jambo la busara zote zishikanishwe ziangaziwe pamoja. Kuna sheria za kufurusha watu, sheria za ardhi ya umma na sheria za watu ambao wamehujumiwa. Sheria zote zikusanywe na kuwekwa pahali pamoja ili mtu akitaka kuangalia sheria za ardhi, asiwe anaenda kwa kitengo hiki na kile na kuzunguka huku na kule. Atakuja kwa hizi sheria za ardhi ambazo zimeletwa pamoja. Ataziangalia na kuzisoma kuanzia sheria za ardhi zenyewe, sheria za mambo ya vile wengine wamefanyiwa tangu hapo awali, sheria za kufurushwa kwa watu na sheria za umilikaji. Tukiangalia yale ambayo yanaendelea nchini hivi sasa, ule ufisadi uliopo na vile watu wamejipatia stakabadhi na vyeti vya mashamba, utapata kuwa moja wa vitu ambavyo sheria hizi zinapaswa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa watu hawataendelea kunyanyaswa na kunyang’anywa mali yao."
}