GET /api/v0.1/hansard/entries/641844/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641844,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641844/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nimesikia ombi la mwenzangu ambaye ni wakili na namheshimu sana. Nashukuru kwa kuwa haujakataa hilo ombi, ila umelichukulia maanani. Vile alivyosema kuwa anaona kweli nafaa kuwa gavana, namshukuru na naomba kuwa Mungu azidi kulirehemu na kulibariki ombi lake. Tutakutana wakati mwingine. Ni muhimu tuangalie kuwa hizi sheria ambazo tumezipitisha hapa na ambazo tutazipitisha tukipata nafasi, Inshallah Mungu akipenda, ziwe sheria ambazo zitaendesha nchi yetu isije ikapata matatizo kwa sababu ya ardhi. Langu la muhimu ni kuangalia vipi tutakavyofanya na ile rasilimali tulionayo. Vile ilivyo, itabidi wale watu ambao wamefanyiwa maovu tangu hapo awali watafute mbinu zingine za kufuata jopo ambalo ni la ardhi ili waweze kuhakikisha kuwa malalamishi yao na zile dhuluma ambazo wametendewa zimefikishwa. Malalamishi hayo ni kama yale nilioyanukuu mwanzo. Kwa mfano, maovu ambayo yametendewa watu wa Taita, ambao ardhi yao yote iko katika mbuga ya kuhifadhia wanyama. Hatukuweka mikakati mwafaka ambayo ingehakikisha kuwa hali waliojikuta inarekebishika kivipi. Namshukuru Mwenyeketi wa Kamati ya Ardhi alivyoifafanua Sheria tuliyofikiria itakuja inayobainisha watu watachukua kiasi kipi cha ardhi. Alieleza kuwa haitakuwa busara kusema tunaweka vipimo kuwa mtu awe na ekari tano, kumi au elfu moja ya shamba kwa sababu inalingana na sehemu aliyoko. Tuliona haifai kuweka viwango vya ardhi ambayo mtu anaweza kukaa nayo. Lakini tukisema hivyo, haimaanishi kuwa sasa watu wanapata ruhusa ya kunyang’anya wenzao ardhi, ili wawe ni wao pekee yao ndio watachukua ardhi. Settlement schemes ni za wale watu ambao wako katika eneo hilo, lakini sheria ilivyo inasema kuwa watu wanaweza kuja wakagawanya hiyo ardhi na kuishi hapo -ilhali wenyeji wanakosa ardhi hiyo. Hizo ndizo dhuluma ambazo lazima zitafutiwe mbinu ya kuzirekebisha. Nikielewa umuhimu wa ardhi, tutajibidiisha tuwezavyo kuhakikisha kuwa haya marekebisho yote ambayo watu wameyaomba na Wabunge wanayaomba yachangiwe kwa undani ili sheria hizi ziwe mwafaka. Marekebisho haya yakipitishwa, hizi sheria zitakuwa za kuungwa mkono na yasipopitishwa, basi tutakuwa na shida. Kama nilivyosema tangu hapo awali, mimi ni mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi na naelewa kinachoendelea. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu nikijua marekebisho yanakuja. Naomba mnitakie kila la heri kwa malengo yangu ya baadaye."
}