GET /api/v0.1/hansard/entries/642018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 642018,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/642018/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukran, Naibu Spika wa Muda. Ninaiunga mkono Hoja hii inayogusia maisha ya wananchi wetu kule nyanjani. Wakati umefika wa kutambua haki za binadamu. Ni makosa sana kuwa vijana wetu wanapotaka kujisajili kule nyanjani wanaambiwa hawawezi kujisajili kuwa wapigaji kura kwa sababu hawana vitambulisho, bali wana stakabadhi za kungojea vitambulisho. Kuwa na kitambulisho ni haki yetu. Pia, kujiandikisha kama mpiga kura ni haki yetu. Ingekuwa bora kama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka na wizara inayohusika na mambo ya vitambulisho wangeweza kukaa pamoja na kuwa na uwiano kwamba wakati vijana wanapopewa vitambulisho ama stakabadhi za kungojea vitambulisho, waweze kujiandikisha kama wapigaji kura. Wakati Serikali ilipoanza kutoa vitambulisho humu nchini, hakukuwa na mpangilio mrefu. Mtu alihitajika kujaza fomu zake zote, na akimaliza anapigwa picha na kupatiwa kitambulisho chake. Sijui ni makosa gani yalitokea, ama ni ufisadi tunaozungumzia ndio maana hakuna mtu anayeweza kuenda katika kituo cha usajili ili apate kitambulisho mara moja. Inachukua hata mwaka mzima kwa mtu kupata kitambulisho chake. Bunge hili lilipitisha sheria kwamba hata hiyo stakabadhi ya kungojea itambuliwe kuwa ni stakabadhi ambayo inaweza kumpa mtu ruhusa ama nafasi ya kuweza kujisajili katika upigaji wa kura. Zaidi ya hayo, utakuta kuwa zile herufi zilizoandikwa katika stakabadhi za kungojea vitambulisho ni nyingi na zinachanganya. Mtu anasahau stakabadhi hiyo na inakua vigumu kuikumbuka. Pia, wanaoziandikisha, waweze kuangalia mbinu mpya za kupunguza herufi zile ndio mtu awe na urahisi wa kukumbuka nambari yake hata kama hajabeba stakabadhi yake na apate huduma mahali popote anapohitaji. Ningependa tume huru ya uchaguzi na mipaka ianze kuwatembelea wanafunzi shuleni kwa sababu wanafunzi hawawezi kuacha masomo na kwenda kwenye afisi ili wasajiliwe. Ninaiunga mkono Hoja hii nikiamini kwamba sheria itaweza kutekelezwa ya kuwawezesha watoto wetu kujisajili kama wapigaji kura. Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}