GET /api/v0.1/hansard/entries/642029/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 642029,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/642029/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningependa Mhe. T.G. Ali ajue kwamba hiyo ndiyo sababu ya kuibadilisha sheria hiyo. Nilipokuwa kule Malindi nilifuatwa na vijana wanaofika 2,000, wakiwa na maua yao wakipiga kelele; wakifikiria kwamba mimi ni mfuasi wa KADU Asili, rafiki yangu, Mhe. Gunga. Inaonekana kwamba kama vijana wale wangelipata ruhusa ya kupiga kura – wale wakiwa vijana kutoka Jilore peke yake, hatujui Malindi nzima kulikuwa na vijana wangapi waliokuwa na kadi za aina ile – nina hakika kwamba badala ya Jubilee nambari kuwa ya pilli ingekuwa KADU Asili. Lakini kwa sababu haki haikuzingatiwa, wale vijana hawakupiga kura."
}