GET /api/v0.1/hansard/entries/643351/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 643351,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643351/?format=api",
"text_counter": 1143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuzungumzia Mswada huu kuhusu sheria ya ardhi. Hili ni suala ambalo ni nyeti na limeleta maafa mengi hapa Kenya. Jamii nyingi zimepigana kwa sababu ya mambo ya mashamba. Sheria hii imekiuka matakwa ambayo Wakenya walizungumzia katika Katiba. Sheria hii inasema kwamba kila pahali ambapo kuna majina “Tume ya Ardhi” yabadilishwe na majina “Waziri wa Ardhi”. Wakenya wengi walipata matatizo kwa miaka mingi waliyofanyiwa na Waziri wa Ardhi ndiposa wakasema kuwe na tume huru ambayo itaweza kutathmini suala la ardhi."
}