GET /api/v0.1/hansard/entries/643352/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 643352,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643352/?format=api",
"text_counter": 1144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika Kifungu cha 42 cha Mswada huu, wameondoa jopo ambalo liliwekwa katika kaunti zetu kutathmini masuala ya mashamba ilhali bodi hii iliwekewa watu ambao wametoka sehemu zile na wanajua masuala ya ardhi. Kifungu cha 44 cha Mswada huu kinazungumzia mambo ya dhuluma za kihistoria na kulikuwa na Mswada kamili ambao ulizungumzia mambo hayo. Sasa hivi, tumepewa maneno machache kuonyesha kwamba hizo dhuluma hazina umuhimu wowote ilhali hilo ni suala nyeti ambalo limeleta madhara. Kifungu cha 46 cha Mswada huu kinazungumzia kuwa Tume ya Ardhi itachaguliwa na Tume ya Kuajiri Wahudumu wa Umma. Itakuwaje tume ichague tume nyingine? Hilo ni suala la kikatiba; kisheria ni kosa. Tume ilikuwa inateuliwa na Rais, majina yanaletwa Bungeni, Wabunge wanayajadili na wanawachagua makamishna ambao watakuwa katika tume hiyo. Katika Kifungu cha 43, aya ambayo ilizungumzia jinsi tutakavyotatua utata wa mambo ya mashamba katika kaunti zetu imetolewa. Hawakuweka njia mbadala ambayo tunaweza kufuatilia suala hili. Vile vile, jambo la ugatuzi limezungumzia suala la ardhi lifike kule chini mashinani katika kaunti. Hivyo basi lazima kuwe na jopo ambalo litashughulikia masuala ya kaunti lakini katika vifungu vya 42 na 43, mambo hayo yametolewa. Kifungu cha 96 cha Mswada huu kimezungumzia settlement schemes, yaani watu waliokosa makazi wanaweza kupewa makazi mahali fulani. Hilo lilikuwa ni jukumu la Tume ya Ardhi lakini sasa jukumu hilo limepewa jopo linaloitwa kwa Kiingereza Land Settlement Boardof Trustees . Mambo kama haya yamekuwa yakitumiwa tangu jadi kuwanyanyasa wananchi wengi hususan kule Pwani na sehemu za Bonde la Ufa. Hatuwezi kutengeneza sheria mama ambayo ni Katiba kisha tutafute sheria nyingine za kuua Katiba kupitia njia ambazo si sawa ili watu warejeshe sheria ile ile yao ama dhuluma zile zile ambazo watu wengi wamefanyiwa katika suala la ardhi. Kama kweli tunataka kuleta The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}