GET /api/v0.1/hansard/entries/643355/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 643355,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643355/?format=api",
"text_counter": 1147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "ambayo yalikuwa katika Tume ya Ardhi yanasemekana yatapatiwa Waziri wa Ardhi. Yatarudi yale yale ya Waziri kukaa katika afisi yake Nairobi agawanye vipande vya ardhi awapatie awatakao na watu ambao wako mashinani katika makazi yale wakose ardhi. Hatutakubali katu. Ikiwa kweli tunataka kuambatisha sheria kwa mujibu wa Katiba, lazima tuwe wangwana na wakweli kama Wakenya kwamba hatutataka tena umwagikaji wa damu na kuona Wakenya wakifurushwa ovyo ovyo. Mswada wa Eviction Bill ulikuwa umetengezwa kupitia Land Act ambayo iko lakini hata Mswada huo pia umefanyiwa marekebisho na kuwekwa katika sheria hii kwa pamoja. Sheria hii imechanganya sheria nyingi na kuziweka pamoja. Mkenya ambaye hana elimu ya juu ya kujua masuala haya hawezi kuelewa sheria hii. Hii yote ni kwa sababu kulikuwa na ukora wa kuweka vipengele vya kurejesha nguvu kule zilikotoka. Sisi kama Wakenya tunaamini kwamba Serikali iliyo sasa inataka kuwapatia Wakenya makazi na kuondoa mzozo wa ardhi. Kama kweli inataka kuondoa mzozo wa ardhi, Mswada huu hautatufaa na utazidisha vita katika Jamuhuri yetu ya Kenya. Tunajua kuna ugatuzi na katiba ambayo sisi wenyewe kama Wakenya tumeipitisha ili iwe na nguvu na kusiwe na mtu ambaye atatumiwa kwa njia moja au nyingine kuwanyang’anya watu mashamba. Mswada huu pia umemuwezesha waziri awe na nguvu za kutathmini mashamba ambayo yamekuwa na utata. Jambo hili ni hatari kwa sababu wale walioibiwa mashamba hawataregeshewa. Mambo yatakuwa yale yale na mkondo utakuwa ni ule ule. Wakenya bado watapata shida. Naibu Spika wa Muda, ninawaomba Wabunge wenzangu tusiangalie chama na tusiangalie tofauti zozote ila tuangalie kule mashinani tunakotoka. Tuangalie nchi yetu kule inakotoka kwa suala la mashamba. Suala la mashamba ni nyeti. Tuachie zile taasisi ambazo sisi kama wakenya tumezibuni, tumezipendekeza kupitia Katiba yetu na kupitia zile sheria nyingine ambazo ziko sasa za kusaidia masuala ya ardhi."
}