GET /api/v0.1/hansard/entries/64344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 64344,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/64344/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Waititu",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Water and Irrigation",
    "speaker": {
        "id": 147,
        "legal_name": "Ferdinand Ndung'u Waititu",
        "slug": "ferdinand-waititu"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, ninaomba kujibu. (a) Ninafahamu ya kwamba wakazi wa eneo la Samburu wamekumbwa na shida kubwa ya uhaba wa maji kutokana na hali ya ukame ambayo imekumba maeneo ya kaskazini, mashariki na sehemu nyingine za Jamhuri ya Kenya. Ukame huu umeathiri sehemu nyingi huku maji katika visima yakipungua na mabwawa ya maji yakikauka. (b) Wizara yangu, kupitia kwa Northern Water Services Board, imeandaa njia kabambe za kusambaza maji katika eneo la Samburu kutumia malori huku usambazaji wa maji kutoka kwa visima na mabwawa ukiendelea. Eneo la samburu litanufaika na shilingi milioni kumi ambazo Wizara yangu imetenga ili kudumisha huduma ya maji wakati huu wa ukame. Wizara yangu imeteua kamati nne ambazo jukumu zao ni kushughulikia juhudi ya kurekebisha visima kwa dharura katika maeneo ambayo imeathiriwa."
}