GET /api/v0.1/hansard/entries/64345/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 64345,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/64345/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, inaonekana Waziri Msaidizi hajaelewa kabisa kuwa watu wako na shida ya maji. Sehemu hizi zote ziko na shida ya maji. Kwa sasa, watu hawana njia yo yote ya kupata maji. Lori ambazo Waziri Msaidizi amesema kuwa zinatumiwa kupeleka maji, hazijaonekana. Kuna sehemu ambayo hata chakula ikipelekwa sasa hii, watu hawana njia yo yote ya kupata maji. Mifugo inakufa kwa sababu ya kukosa maji. Hakuna lori yo yote ambayo inasambaza maji na visima vimekauka vyote. Ningemuomba Waziri Msaidizi aelezee kwa njia ambayo inaeleweka."
}