GET /api/v0.1/hansard/entries/643547/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 643547,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643547/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Muda huu wanaouliza wa miezi mitatu kuweza kumaliza maswala yale ambayo walikuwa wametumwa kuyatekeleza inafaa uongezwe. Bila shaka ni sawa kwa Bunge hili la Kumi na Moja kuweza kuwaongezea miezi hiyo mitatu, ili waweze kutekeleza jukumu lao na kulikamilisha inavyotakikana. Nakubaliana na wenzangu ya kwamba tume ya kusimamia maswala ya mahakama imekuwa na matatizo mengi. Wakati ni sasa sisi tuweze kuangalia sheria iliyotengeneza tume hiyo ili tuweze kutengeneza kuwa wale wanachama wa tume waweze kufanya kazi pasipo kuchanganyikiwa na kazi zile zao za uwakili na ujaji. Katiba imewapatia nafasi ya kukaa pale, lakini inawachanganya kwa sababu vile vile wanaendelea na shughuli zao na inawabidi pia wafanye kazi kufuatana na vile Katiba ilivyotaja. Binadamu si kamili. Mara kwa mara, sio rahisi kwa mtu kuweza kutenganisha lililoko rohoni na lililoko mbele yake. Hivyo basi, nakubaliana na wenzangu kuwa hata hiyo sheria ya hiyo tume ya kusimamia maswala ya mahakama, itabidi tuiangalie ili tuweze kurekebisha pale ambapo wanachama wako na matatizo . Miezi mitatu si muda mrefu na kwa vile hawahitaji kuongezewa fedha za kufanyia kazi, basi mimi naunga mkono kuwa wapatiwe muda huu wa miezi mitatu waweze kumalizia maswala walioanza kufanya. Ukweli ni kuwa ni rahisi kwa wale ambao hawafanyi kazi hii kuona kuwa labda hawajafanya kazi. Mimi najua kuwa kazi imefanyika na sio rahisi kwa sisi sote kusema kuwa kazi hiyo ingekuwa nyepesi. Kazi hiyo ni nzito na haikuwa nyepesi. Nataka kuwapa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}