GET /api/v0.1/hansard/entries/64364/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 64364,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/64364/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Waititu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 147,
"legal_name": "Ferdinand Ndung'u Waititu",
"slug": "ferdinand-waititu"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, Wizara yangu, kutoka makao makuu, hutoa idhini ya kutumia pesa kwa afisa mkuu wa maji wilayani. Akishapata AIE, anakuwa na ruhusa ya kutumia pesa kulingana na mahitaji yao. Tumeshatuma malori mawili ya kusafirishia maji, na tayari yako huko. Tumetuma lori moja kutoka kwa kikosi cha Askari Tawala (AP), ambalo ni Four Wheel Drive, ndiyo liweze kupita kwenye barabara mbovu. Pia tumetuma lori lingine kutoka kwa Idara ya Huduma kwa Vijana wa Taifa (NYS). Tumeshawatumia pesa ambazo watatumia kukomboa malori na kununua vipuri vya magari."
}