GET /api/v0.1/hansard/entries/643678/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 643678,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643678/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 769,
        "legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
        "slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mswada uliopo mbele yetu wakati huu wa kusawisha idadi ya akina mama katika Bunge hili ni muhimu sana. Tunafurahi tunapofikiria jinsi tutakavyoweza kuwaongeza wanawake katika Bunge. Sio katika Bunge peke yake bali pia katika ajira na hata huko mashinani wanaweza kusimamia mahali popote. Tunafaa kuwahusisha akina mama. Tunapaswa kujua kuwa akina mama ndio wenye idadi kubwa zaidi. Sisi Wabunge tunapigiwa kura na akina mama. Pili, sisi sote tumetoka kwa akina mama. Ni wazazi wetu, dada zetu na watoto wetu. Kwa hivyo, tunapowafikiria akina mama, tuangalie kama sisi Wabunge tuna watoto wasichana. Je, tungetaka watoto wetu wawe akina nani? Je, hatungetaka wawe Wabunge katika miaka ijayo wakati hatupo Bungeni? Ni lazima tufanye juhudi ili idadi ya wanaume na wanawake iwe inalingana kama ilivyo katika nchi nyingine. Tunafaaa kuangalia wakati Kongamano la Beijing lilipofanyika. Mikutano iliyofuatilia ilikuwa mitatu huko Uingereza (UK), Copenhagen na Beijing. Mkiangalia katika historia, mtaona kwamba baada ya Kongamano la Beijing, kulitokea Serikali 189 ambazo ziliunga mkono pendekezo la akina mama wasawasishwe na wanaume katika nyadhifa zote. Hili si jambo jipya Kenya. Ni jambo linaloendelea. Lazima tufikie usawasishaji wa akina mama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}