GET /api/v0.1/hansard/entries/643679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 643679,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643679/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 769,
        "legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
        "slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
    },
    "content": "kulingana na Malengo ya Milenia. Muda wa malengo haya utakapotimia, lazima idadi hii iwepo kwa sababu sio Kenya peke yake bali dunia nzima. Sisi tutaweza kuachwa vipi nyuma? Sisi akina mama hatuombi. Ni jambo ambalo linaendelea. Ni haki yetu pia sisi kupatiwa nafasi. Katika hili Bunge, tunafurahi sana kwani tunaungwa mkono na wenzetu wanaume ambao wana watoto wasichana ambao wangetaka waingie katika Bunge hili na pia katika Bunge za Kaunti. Tunaomba tupatiwe nafasi na tutawaonyesha kuwa akina mama wanaweza. Akina mama wanaweza kushikilia nyadhifa zozote. Tunataka akina mama huko mashinani tunakotoka wasijihisi kama wameachwa nyuma. Wakijihisi kama wameachwa nyuma ilhali tunawawakilisha katika Bunge, hiyo itakuwa kutupeleka nyuma. Akina mama wanaweza kusema kuwa hawana wawakilishi Bungeni. Kama hawana wawakilishi katika Bunge, basi sisi tufanye nini? Mbona tusiwashike mkono kama wenzetu katika Bunge? Kwa hivyo, wakati sio mwingine ila ni huu. Tungetaka sehemu mbili kati ya tatu iwe ya akina mama."
}