GET /api/v0.1/hansard/entries/643892/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 643892,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/643892/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hiyo nafasi ya muda mdogo japo nilikuwa nataka kuwa na muda wa kutosha. Ukweli ni kwamba tungetaka sana kupitisha Mswada huu. Kwa wakati ujao, tungetaka tuwekewe sehemu nyingine inayoonyesha kuwa katika majimbo na zile sehemu ambazo pesa zinakusanywa, ni kiwango kipi cha pesa kimekusanywa ili wakati wanapewa pesa zingine, tuangalie ni vipi tutawapa pesa kwa sababu saa hivi tunatoa pesa ambazo hatuelewi zitatumika vipi. Upande wa unyunyizaji wa maji katika mashamba ningeomba tuweze kusimamia sekta hii iendelee katika Galana kwa sababu ni moja kati ya sehemu ambazo zinaweza kulisha nchi hii."
}