GET /api/v0.1/hansard/entries/644387/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644387,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644387/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii ili kuunga mkono Hotuba ya Rais. Nachukua fursa hii kumpongeza Rais wetu kwa kusimama kidete ingawa alisumbuliwa na kulikuwa na changamoto ya sauti za firimbi ndani ya Bunge. Hata hivyo, alistahimili na kusoma Hotuba yake mpaka mwisho. Pia, nawashukuru Wabunge wa Mrengo wa Jubilee ambao walikuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati Rais alikumbana na changamoto ya sauti ambayo hatukuelewa ilikuwa ya nini. Ajabu ni kuwa Wabunge walianza kupuliza firimbi bila kumpa Rais nafasi kutoa Hotuba yake. Hakuna njia nyingine Rais wetu anaweza kuongea na wananchi wake isipokuwa kufika katika Bunge la Taifa na kuhutubia Wabunge ambao walichaguliwa na wananchi wa Kenya. Hakuna njia nyingine isipokuwa hiyo. Nachukua nafasi hii kumpongeza sana Rais wetu. Amekuwa akiongea na watu wake ambao walimchagua kuwa Rais wa nchi hii. Amekuwa akiongea nao kwa njia ya Hotuba katika Bunge la Taifa. Bw. Spika wa Muda, ningependa pia kuchukua nafasi hii kuongea juu ya matumizi ya pesa katika serikali za kaunti. Matumizi ya pesa za kaunti yanatuhusu sisi viongozi. Pesa ambazo zinapelekwa katika serikali za kaunti ni kwa minajili ya mwananchi wa nchi hii. Kwa hivyo, itakuwa ni aibu sana wakati hesabu ya pesa ambazo Seneti imeidhinisha zitumwe kwa serikali za kaunti inatolewa na kupatikana kwamba hazikuwasaidia mwananchi kwa njia yoyote. Kwa hivyo, ni vyema ikiwa umechaguliwa kuwa kiongozi, jinsi magavana walivyochaguliwa katika kaunti zao, kuongoza na kuangalia jinsi rasilmali zetu zinavyotumika. Itakuwa aibu sana iwapo itapatikana kuwa pesa za wananchi zinatumika kwa njia isiyofaa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}