GET /api/v0.1/hansard/entries/644504/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644504,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644504/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii niunge mkono Mswada huu. Kando na kuunga mkono Mswada huu ninataka kusema kuwa Wakenya wengi sana wana matumaini na benki zetu za Kenya. Lakini matumaini hayo kwa wale wanaoweka pesa zao huko yanawaletea shida. Benki nyingi sana hapa nchini Kenya hivi sasa tunaona zinamilikiwa na matapeli. Nikisema hivyo, karibuni ilikuwa Benki ya Imperial na juzi Benki ya Chase. Wananchi waliokuwa wanalia kwa sababu wameweka pesa zao huko ni wafanyi kazi wadogo. Mpaka saa imekuwa ni shida kuona kuwa pesa zao haziwezi kuwasaidia. Inasikitisha sana kuona kuwa mwananchi wa kawaida anaweza kutoka nyumbani kwake na kuelekea kwa benki zetu za Kenya kuweka pesa zake akiamini kuwa ziko mahali salama. Lakini inakuwa hali ngumu kwa mwananchi yule ambaye ameweka akiba yake huko kuamka asubuhi moja na kuambiwa benki imefungwa ilhali alikuwa anajiendeleza. Anarudi katika hali ya umaskini. Afadhali hao wananchi wafikirie njia na mbinu za zamani. Badala ya kupeleka pesa kwa benki afadhali waziweke chini ya godoro mahali ambapo ni imara zaidi kuliko kuziweka kwa benki leo halafu kesho ama kesho kutwa usikie benki imefungwa. Ni muhimu Serikali ije na vidhibiti kamili vya kuona ni namna gani watakuwa na mwongozo sawa katika hizi benki zetu ili wakati watu wanaweka pesa zao huko hakuna shida. Kitu ambacho kinanishangaza zaidi ni kuona mwananchi wa kawaida akienda kukopa pesa katika benki zetu. Akipewa mkopo na achelewe kidogo kuulipa, unasikia mtu amepelekwa kwa wadhibiti wa benki. Hataweza kufanya biashara katika benki yoyote nyingine. Huyo ni mwananchi wa kawaida. Lakini akiwa mkurungezi wa benki, tunaambiwa hiyo ni kukopa ndani kwa ndani. Unaona mtu yule anakopa hata bila dhamana. Wanasikizana leo tu na kuchukua shilingi bilioni moja au moja na nusu. Bila vidhibiti zaidi, wananchi wa kawaida wanapata ugumu kujikimu kibiashara. Ninaunga mkono Mswada huu na kusema kuwa Serikali yetu ni lazima isimame kidete na kuona kwamba benki zetu zinaweza kudhibitiwa ili wananchi waweze kupata dhamana ya pesa zao na wajiendeleze kimaisha. Kwa hayo machache, ninakushukuru sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nichangia Mswada huu."
}