GET /api/v0.1/hansard/entries/644527/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644527,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644527/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu ambao umeweza kufika wakati ambao Wakenya wanateseka. Wakenya hukaa wakiwa na vipeni vyao hususan kina mama ambao wameamka na biashara ndogo. Wanatafuta mahali pa kuwekeza vipeni vyao vidogo ili waweze kupata mkopo waendeleze biashara. Lakini unakuta katika zile benki zetu tunazozitegemea za Serikali, ni vigumu kupata mkopo kwa sababu wanahitajika udhamana wa hali ya juu. Wanapokimbilia hizi benki ndogo ambazo zinabuniwa za kisasa zenye riba ya chini, inafika wakati wanarudi kujuta kama hivi sasa tunalia Chase Bank na Imperial Bank zimefungwa."
}