GET /api/v0.1/hansard/entries/644528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644528,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644528/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Katika eneo Bunge langu, kuna mwekezaji ambaye alikuwa ameamua kushirikiana na wananchi katika upande wa baharini ili waweze kuanzisha mradi ambao ungekuwa ni historia katika Afrika wa Well Shark ambao kwa Kiswahili tunamwita Papa Shilingi. Pesa ziliwekwa katika Imperial Bank. Leo hatuelewi kama Imperial Bank itaweza kufufuka ama itakuwa ni vipi. Kwa hivyo, Mswada huu umeletwa kwa wakati unaofaa lakini tunajiuliza Benki Kuu ya Kenya iko wapi wakati benki hizi zinakuja kutapeli wananchi? Banki kuu ya Kenya ndio macho ya mwananchi na Serikali. Mbona wakuu wa Benki Kuu wamenyamaza wakati watu wanatapeliwa? Hakuna hatua ambayo inachukuliwa kwa wale wanaotapeli wananchi. Kwa hivyo, Mswada huu utatusaidia kurekebisha na kuweka sheria mwafaka ambazo zitasimamia haki za mwananchi kupitia maeneo inayohusiana na pesa wanazoweka katika benki zetu."
}