GET /api/v0.1/hansard/entries/644529/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644529,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644529/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Pia, tungependa Bunge hili, kupitia Kamati yetu ambayo inahusika na mambo ya fedha, ihakikishe kuwa Benki Kuu ya Kenya na Waziri wametuelezea ile pyramid scheme ambayo iliwatapeli Wakenya fedha ilienda wapi. Kule Kwale, kina mama na wazee wengi walikufa kwa kiwewe baada ya ile pyramid scheme kuanguka. Tunafaa kujua kufikia leo pesa hizo ziko wapi na ni lini wananchi wetu watarudishiwa pesa zao. Watu walikimbia kuweka pesa kwa wingi kila siku na kila uchao wakifikiria kwamba wakati umefika wa kujinasua katika matatizo waliyo nayo ya kiuchumi. Kumbe walipeleka pesa zao katika midomo ya papa na zilimezwa na mpaka leo hatujui tutaelekea wapi."
}