GET /api/v0.1/hansard/entries/644667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644667/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono Hoja ya Mhe. (Dkt.) Ottichilo ambaye ameona umuhimu wa sisi kuzungumzia suala la mazingira. Suala hili limekuwa donda sugu ambalo Wakenya wote wanatakikana kuliangazia. Suala hili limetajwa kwenye Katiba katika Vipengele vya 42, 69 na 70, japo kama Wakenya, tumechukulia mazingira kama jambo la dhihaka na mchezo na wala sio jambo la kulindwa na kutunzwa. Wakenya wengi wanaugua magonjwa tofauti. Kule mashambani, mifugo wetu wanakula karatasi zinazotupwa na wanakufa. Mbuzi wengi wamekufa kwa sababu ya kutafuna karatasi badala ya nyasi. Ni jambo la kusikitisha kuwa kama Wakenya, tunafikiria kwamba inatosha tu kufagia nyumba na kutupa takataka hapo nje. Tukisafiri ulimwengu mzima, tunaona na kufurahia usafi tunaouona kule. Lakini tunaporudi nyumbani, hatujali usafi wa mazingira na maeneo tunayoishi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}