GET /api/v0.1/hansard/entries/644668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644668,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644668/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Sio mara ya kwanza kwa Mhe. (Dkt.) Ottichilo, ambaye anaelewa masuala ya mazingira, kuleta Hoja kuhusu mazingira. Lakini mara nyingi ametaka kubadilisha sheria ili kutekeleza yale ambayo yako kwenye Katiba yetu ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanaishi kwenye mazingira yanayofaa na kudumisha mazingira haswa wakati huu ambapo masuala ya mazingira yameharibu mambo mengi hapa duniani. Ufagio ni chombo kinachotumika kwa usafi na unatakikana kuwa rafiki wa kila mtu. Ufagio pia ni mti ambao hauwezi kukuzwa kwenye maeneo ambayo hayafai. Hivyo basi, Hoja hii ya kuwa siku moja kwa mwezi Wakenya wote wajitokeze kusafisha miji yetu ili tuishi kwa mazingira mazuri ni Hoja muhimu na ningependa kuwaomba wenzangu kuipitisha haraka iwezekanavyo ili suala liweze kutekelezwa. Rais alipopata kiti kwa mara ya kwanza, alionyesha umuhimu wa kuweka mazingira yetu safi kwa kufagia wakiwa na Gavana wa Nairobi. Lakini hatukufuatia kufanya yale ambayo aliyafanya. Huyu Gavana Kidero ambaye ndiye anasimamia mji wa Nairobi ni kama alisahau suala kubwa analopaswa kuliangalia. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Nahimiza kuwa vipengele 42, 69 na 70 vya Katiba vitekelezwe vilivyo ili tuweze kuweka mazingira yetu yawe masafi."
}