GET /api/v0.1/hansard/entries/644679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644679,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644679/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Ottichilo. Tukiangalia hali ya mazingira katika nchi yetu ya Kenya, wakati umefika sisi kama Wakenya tuangalie namna tutakavyobadilisha mazingira yetu. Itakuwa vyema kama akina mama ambao wanafanya biashara katika barabara zetu kuu wataangalia mazingira baada ya kufanya biashara kabla ya kwenda nyumbani na kuacha sehemu ambayo wametumia kuwaletea chakula kila siku ikiwa safi. Ingekuwa vyema zaidi kama wangeangalia namna ya kutoa takataka hizo na kuzichoma katika hali inayotakikana ili tulinde mazingira yetu. Wakati mmoja, Nairobi ilikuwa inajulikana kama sehemu yenye rangi ya kijani kibichi katika eneo lenye jua sana. Lakini siku hizi, Nairobi ni jiji limejaa plasitiki, mikebe na karatasi. Huwezi kuona eneo lolote lililopandwa nyasi. Sasa, lazima utafute maeneo yenye nyasi. Naunga mkono kauli ya Mhe. Milly. Tuangalie kama itakuwa siku ya Alhamisi ili sisi sote tuungane kusafisha mazingira yetu yawe masafi. Siku hiyo ya Alhamisi itawawezesha pia ndugu zetu Waislamu na ndugu zetu ambao wanaenda katika kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) siku ya Jumamosi kuungana mikono pamoja ili tusafishe mazingira yetu katika nchi yetu ya Kenya. Itakuwa vyema zaidi kama viongozi pia wataonyesha mfano mzuri. Tunapaswa kuanza katika maeneo yetu na sehemu tunazoongoza. Tushike ufagio, tupande miti na kuchoma karatasi ili nchi yetu yote na kaunti zetu 47 ziwe safi."
}