GET /api/v0.1/hansard/entries/644730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644730,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644730/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Kwanza tunampongeza Sen. Wetangula kwa ujasiri wake wa kuamua kwamba anaweza na angependa kuwa Rais wa nchi hii. Huenda wengine wetu tukafuata mkondo huo na kutangaza msimamo wetu. Hata hivyo, jambo lilotokea huko lilikuwa la aibu na halikupendeza macho ya Wakenya wengi. Ni aibu kuona mkutano kama huo ukiingiliwa na majambazi jinsi ilivyofanyika siku hiyo. Je, vitoamachozi ambavyo vilitumiwa vilikuwa vimechapwa muhuri gani? Kulikuwa na muhuri wa Serikali na vilifikaje huko? Maswali hayo ni lazima yajibiwe. Ningependa kuwasihi viongozi wetu wa Upinzani kuketi pamoja na kuongea mambo yao polepole. Hii ni kwa sababu sisi wanachama wa muungano wa CORD hatupendezwi na mambo kama hayo. Lazima niseme kinagaubaga kwa sababu sisi hatupendezwi na vituko kama hivo tulishuhudia siku ya Jumamosi. Kwa nini viongozi watatu wa muungano wa CORD hawawezi kukaa pamoja na kutafuta njia nzuri ya kupata kiongozi? Kwa nini mnavunja muungano wa CORD? Imefika wakati ambapo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}