GET /api/v0.1/hansard/entries/644928/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644928,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644928/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kwenye Upinzani wasije wakafuata mfano ambao ulionyeshwa na Wabunge kadhaa. Hiyo sio sera ya Upinzani bali ni sera ya watu binafsi. Nilikuwa mmoja wa Wabunge kutoka Upinzani. Nilikaa kitako na kuisikiliza Hotuba ya Rais kutoka mwanzo mpaka mwisho. Nilitaka kuielewa, kuichunguza na kutoa dhiki endapo ningekuwa nayo wakati ukifika; wakati ambao umewekwa wakfu kwa Mabunge haya kila wakati kujadili Hotuba ya Rais aitowapo ndani ya Bunge. Huwa haichukui siku moja au siku mbili bali siku tatu ili ujitonde vile unataka na hakuna atakayekuuliza. Hivyo ndivyo sera na desturi ya wasomi na watu wenye hekima ilivyo. Ningependa wenzangu waheshimu Katiba na Sheria za Bunge. Mwanzo, Rais alianza kwa kutuambia mambo ya Uhuru. Wakati wa Uhuru, wengine wetu tulikuwa wakubwa kidogo. Tulikuwa tumezaliwa na kujua yaliyokuweko wakati wa ukoloni, tulifurahia Uhuru na mwito uliotolewa wakati huo na Rais wa kwanza wa nchi hii hasa kwa umoja wa taifa. Wakati huo, kulikuwa na upendo. Kulikuwa na vyama viwili vikuu; the Kenya African National Union (KANU) na the Kenya AfricanDemocratic Union (KADU). Wakati huo, walifikiri kwamba wanaleta umoja, lakini baadaye waligundua kosa walilofanya. Hadi mwaka wa 1966, ndivyo tukaanza kuona haya na haya, kukaja kifo cha marehemu Tom Mboya mwaka wa 1969. Siasa zikaanza kunoga nchini Kenya. Tunashukuru Rais mstaafu Moi aliyekuwa Rais hadi mwaka 2002 ambapo kitengo cha 2(a) kilitolewa katika Katiba na kutupa nafasi tena ya kuwa na vyama vingi. Ndipo sasa tunapata nafasi hii ya kuongea mambo ya Hotuba ya Rais au hata kukufuru tukitaka."
}