GET /api/v0.1/hansard/entries/644930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644930/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, Rais alidokezea zaidi migogoro iliyokuwepo mwaka 2007/2008 baada ya uchaguzi. Kulikuwa na vita na watu zaidi ya 1,000 wakauawa na wengine karibu 6,000 wakaathirika kwa kupoteza nyumba na mali. Mimi mwenyewe nikiwa Waziri wakati huo, kwa siku mbili tu Jijini Migori, nilipoteza mali ya Kshs25 milioni iliyoharibiwa kwa kuchomwa au kubomolewa kwa sababu wakati huo nilikuwa ndani ya Serikali na nilihifadhi Wakikuyu kwa nchi ya Wakuria. Ndivyo ilivyokuwa na ni aibu. Niliwapa hifadhi, utulivu na amani lakini nikalipa deni. Ninawapongeza watu wa Migori pia kwa sababu baadaye, walinichagua nikawa Seneta wao na kunituliza moyo kidogo kwamba, mzee, tunajua una uongozi mzuri, sahau yaliyopita. Nikasema mimi nimesahau yaliyopita na ninaganga yajayo. Hata hivyo, kama mimi sasa ninahisi huo uchungu, na wale walioathirika kiasi cha kutokuwa na chochote hata nyumba ya kwenda kuingia, je, wamesahaulika. Tunashukuru Mungu kwamba Naibu wa Rais wa nchi hii pamoja na mwenzake, kijana, wameondolewa minyororo katika mahakama ya International Criminal Court (ICC). Tunashukuru kwamba yuko nyumbani na anafanya kazi bila wasiwasi. Tunashukuru kwamba juma lililopita, tumeona ibada za maombi kanisani. Nafikiri pia kuna maombi makubwa sana yanayoandaliwa Mjini Nakuru, Jumapili ijayo, kwa ajili ya hawa wawili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}