GET /api/v0.1/hansard/entries/644932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644932,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644932/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Swali ni; je, wale walioathirika tutawaombea siku gani? Je, wanahisi vipi tunapotoa hotuba kama zile na kutukuza hawa wenzetu wawili vile walivyoponyoka kutoka kwa janga hili kwa sababu wako kwa uongozi? Je, wanahisi ya kwamba wamesahaulika? Wengine walipata Kshs400,000, wengine Kshs10,000 na ekari moja moja ya shamba. Hata hivyo, ni haki? Kwa hivyo, ni lazima tutafute njia nzuri ya kushukuru Mungu kwa hili jambo na tusije tukafungua vidonda bila sababu. Lazima tuwe na utu wa kumfikiria yule kabaila sana kwa umma, na pia kufahamu kwamba binadamu wote ni sawa na wapate huduma sawa na wale wakubwa. Tunashukuru Bw. Farah aliyetukuzwa na Rais wakati wa Hotuba yake, kwa kujitolea mhanga na kuwaokoa Wakristo ndani ya bas. Mungu airehemu roho yake. Pia, ninawatukuza askari wengi waliopoteza maisha yao wakitusaidia sisi wananchi kutunza na kuilinda nchi yetu kwa usalama. Tunataka Serikali iangalie maslahi ya familia zao kwa dhati wala sio kupiga tu risasi wakati wa mazishi na kusahauliwa. Lazima Serikali iwe na mbinu. Ninafurahi kwamba wakati huu kuna bima ya afya ambayo imeanzishwa kwa askari na ninaamini kwamba jamii za askari walioathirika zitapata malipo ya bima. Hata hivyo, sio mishahara ya kaskazini mwa Kenya tu ndio itunzwe. Ukifika Nyanza, kuna shida na mgogoro ambao labda utaleta shida - Kisiwa cha Migingo. Kila Rais anapotoa hotuba, sisikii akiguzia Kisiwa cha Migingo ambacho kiko Kaunti ya Migori. Ni chetu lakini kimekaliwa na wakoloni mamboleo ambao ni Serikali ya Uganda. Kweli ni mmoja wetu wa nchi za Afrika Mashariki lakini kwa nini kutuchoma macho na vijiti? Swala hili lilifika wapi? Mara tulisikia kwamba kuna tume iliyoundwa ya kuangalia mipaka. Mpaka sasa Kenya hatujui mipaka yetu iko wapi? Mara tuliambiwa kisiwa ni chetu lakini maji na samaki sio ya Wakenya. Tusi kwa nchi yetu! Ingawa jambo hili linaonekana duni, linatuathiri sisi wananchi wa Nyanza Kusini. Bw. Spika wa Muda, Rais pia alidokezea maendeleo yaliyofanywa na kutuambia kuhusu magari 3,000 na vifaa vya matibabu. Hata hivyo, hakutuambia magari ya zamani yalienda wapi. Wakati mmoja, Rais akiwa waziri wa fedha nami nikiwa waziri wakati huo, magari yote aina ya Prado na Mercedes ya 3,000 cc yalikusanywa yote na tukapewa Volkswagen. Mimi na ukubwa wangu huu nilijiingiza ndani ya Volkswagen na kwenda tu. Ni gari nzuri. Tukasema: “Basi! Tumefika.” Yale magari yaliachwa yakazorota mpaka sasa hatujui tulipata faida gani kwa mpango huo. Sasa tena tumeona mashangingi; Prado, V8 na Range Rover zimekuja na ndio sasa magari ya Serikali. Kwa sasa, Kenya ina deni la karibu Kshs3 trilioni. Mzee Kibaki aliacha utawala tukiwa na deni la Kshs680 bilioni. Kwa hiyo miaka michache tumetoka Kshs680 bilioni hadi Kshs3 trilioni. Maana yake sasa ni kwamba, kila mtu ambaye hajazaliwa hata yule ambaye bado ni yai, ana deni. Miaka ya binadamu ni miaka 80. Kama unakula vizuri na unaangaliwa vizuri, utafikisha miaka 90. Lakini, Bibilia inasema miaka 70 na zaidi ya hiyo, ni ya ziada. Umeachia vitukuu na vilembwe deni. Haki iko wapi? Kwa hivyo, lazima tujihadhari kabisa maana vizazi vijaavyo vitatulaumu wale tuliomo uongozini kwa sababu ya kuwapachika madeni kushoto, kulia. Madeni hayo sio kwamba yanatumika kwa kazi ya maana bali ni rushwa ilhali tunaaendelea kulipa. Mkubwa akishikwa anafungwa jela miaka 20, lakini mwnanchi akishikwa kama ameiba kuku huona cha mtema kuni. Utahukumiwa miaka sita kwa kuiba kuku kwa sababu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}