GET /api/v0.1/hansard/entries/644943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644943,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644943/?format=api",
    "text_counter": 251,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ambayo nilikuwa nimeingojea kwa hamu na gamu mchana wa leo. Nilikuwa likizoni lakini nilijua kwamba badala ya kupiga filimbi nitapata fursa ya kuongea na kusikika kwa njia inayokubalika. Nampa hongera Rais wa Jamhuri yetu ya Kenya kwa sababu alionyesha umahiri wake. Sio jambo rahisi wakati unataka kuongea na watu wengine wanataka kukufanya uonekane ni kama huna maana. Ule ulikuwa mtiani mkubwa na kwa hivyo nampa Rais hongera sana. Kulikuwa na wageni kutoka nchi mbalimbali na watoto wa shule katika Bunge letu. Wakenya wengi walikuwa wanaangalia kilichokuwa kinaendelea. Kilichotendeka halikuwa jambo rahisi; ilionyesha ukomavu wa watu walioko Serikalini na Rais. Huu ulikuwa mtiani mkubwa sana. Haikuwa aibu tu kwa nchi yetu ila kwetu sote. Itakuwaje mtu ambaye ni kiongozi abebwe hobela hobela? Itabidi turejelee kipengee kinachohusu kutolewa Bungeni kwa nguvu. Ni aibu kubwa kwa familia ya Waheshimiwa ambao walitolewa Bungeni kwa nguvu. Nguo ya mmoja wao iliraruliwa na hata akuvuliwa viatu. Kulikuwa na wanafunzi Bungeni ambao wanajua Rais kama kiongozi mkuu wa Kenya ambaye anastahili kuheshimiwa. Huo ulikuwa mtihani na funzo kubwa kwetu zote kama Wakenya. Kitendo kama kile cha kumpigia Rais firimbi ni cha aibu and hakifai tena. Ni lazima tuwe na nidhamu. Tulifaa kungojea siku kama ya leo ili tupeane maoni yetu. Waswahili wanasema unafaa kusikiza kisha uamue utakavyo mwenyewe. Hufai kuleta vitimbi na kuonekana na jamii yako ukibebwa kihobela hobela kama gari mbovu. Kitendo kama kile kinaweza kumpata mwanasiasa yeyote na kionekane kwenye runinga na wake au watoto wao. Kwa hivyo, tunastahili kudumisha nidhamu Bungeni. Wakati ule ulikuwa wa Rais kutueleza vile nchi inaendelea. Ni ajabu kwamba hata wanahabari waliyapa uzito zaidi matukio mengine kuliko Hotuba ya Rais. Hawakutueleza umuhimu wa maneno ya Rais. Bw. Spika wa Muda, nina furaha kwamba kesi iliyokuwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai imeisha. Kesi hiyo ilikuwa inatupotezea uzingizi. Sasa tumebakia na shida moja ya wenzetu wakimbizi wa kisiasa. Je, tutawafanyia nini ili wajihisi kuwa pia ni Wakenya ambao wako huru kama Makamu wa Rais na Bw. Sang? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}