GET /api/v0.1/hansard/entries/644953/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644953,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644953/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, Sen. Muthama amenirudisha nyuma. Hata hivyo, ni ombi langu kama Mkenya na mama kwamba waathiriwa wapewe haki. Shida tuliyonayo sasa ni moja si kama hapo awali wakati shida zilikuwa nyingi. Mhe. Naibu wa Rais sasa ametulia. Ninahakika kwamba mambo mazuri yanakuja kwa sababu tunataka sote tuishi pamoja kama Wakenya wa kabila na dini moja ndiposa kila mmoja wetu ajihisi huru katika nchi yetu. Ni ombi langu kuwa wote walioathiriwa katika ghasia za uchaguzi waridhiwe ili nao wajisikie ni Wakenya. Tumekuwa tukiomba na maombi tunayoandaa, ningependa tuwaombee kila mmoja wetu kwani shida tuliyonayo sasa ni ya uwiano na kuishi pamoja kama ndugu na jamii moja. Mara kwa mara, binadamu akifanikiwa humkimbilia Mwenyezi Mungu kwa heshima kutoa shukrani. Kama tujuavyo, tukiomba na kuamini, waathiriwa watafaidika na tutaishi kwa amani. Nina hakika kuwa Mwenyezi Mungu atajibu maombi yetu na tutapiga hatua za kimaendeleo. Sisi kama Wakenya ni lazima tuishi kwa umoja natupige vita sababu zote zinazotutenganisha kama jami moja. Tujiulize jinsi Wakenya ambao nyoyo zao zina majonzi, watasaidika aje. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}