GET /api/v0.1/hansard/entries/644955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 644955,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644955/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, nampongeza Mhe. Rais Kenyatta kwa sababu sauti yake ilikuwa imara na haikutoa kite hata baada ya kupigiwa firimbi ndani ya Bunge. Hatuwezi kusahau jambo hilo kwani tuliona ameimarika na kwamba amekomaa kisiasa. Wengi wetu wangepigiwa firimbi hivyo wangekasirika lakini Mhe. Rais wetu alitulia hadi mwisho wa makelele kisha akatoa hotuba yake. Mhe. Rais ni shujaa, mahiri na hachaguwi nani yuko katika Serikali yake. Yeyote anayefanya kitendo kisichofaa anatimuliwa. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}