GET /api/v0.1/hansard/entries/644956/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644956,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644956/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ninakushukuru kwa nafasi hii uliyonipa ili niweze kuchangia Hotuba ya Mhe. Rais Kenyatta. Sikufika siku hiyo Bungeni lakini nilitazama yote yaliyofanyika katika runinga. Kuna maswala mbalimbali ambayo yalinikera na si kwa sababu za kisiasa bali kwa kuwa mimi ni mwananchi wa Kenya. Niko hapa na nitazidi kuwa hapa mpaka siku aipendayo Mwenyezi Mungu. Bw. Spika wa Muda, kuna mambo yaliyotokea. Mojawapo ni kasheshe iliyotokea Bungeni. Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Kitaifa walizua taharuki. Wengi waliwashambulia na kumlazimisha Spika wa Bunge kuwatimua. Hata mwingine alifukuzwa. Inasemekana kwamba atakuwa nje kwa kipindi cha zaidi ya siku 90. Tunafahamu kwamba kulingana na Kanuni za Bunge hiyo inamaanisha nini. Haifai Spika wa Bunge lolote kuchukua uamuzi wa namna hiyo kwa sababu Mbunge fulani ametoa mapendekezo yake na kuzungumza wazi. Bwana Spika wa Muda, Wabunge waliotimuliwa Bungeni walikuwa wanafanya kazi waliotumwa na wananchi kufanya. Mbali na kuwa Rais wa Nchi, Mheshimiwa Kenyatta sio Mbunge wa Bunge lolote; Bunge la Kaunti, Bunge la Kitaifa au Bunge la Seneti. Akiwa pale, yeye ni mgeni. Kuna wale ambao ni wenyeji. Hao ni Wabunge na wana haki ya kuzungumza na kufanya mambo yote yanayohusu shughuli za Bunge. Lakini, Rais alistahili kustahimili kwa sababu nilishuhudia katika Bunge la Kumi, upande wa ODM ukiwa upande ule na upande wa PNU upande huu; Rais Kibaki alipokuwa akiapishwa tulikaa Bungeni tukichagua Spika na Wabunge wakiapishwa kuanzia Saa nane na nusu za alasiri hadi mpaka Saa kumi asubuhi. Asilimia 75 ya shughuli za Bunge ilikuwa ni kupinga uchaguzi wa Rais kwa kiapo. Hakuna Mbunge alitimuliwa. Mhe. Kibaki alizomewa Bungeni, nikiwa Naibu wa Kiranja, na aliitwa mwizi. Nikiwa mrengo wa PNU nilishuhudia Rais wa taifa akiitwa mwizi. Alitembea pole pole kwa utaratibu mpaka kwenye kiti chake, akaketi na akatulia. Nakumbuka kwamba Waheshimiwa fulani ambao leo ni Mawaziri katika Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, walimkashifu na kumuudhi Mhe. Kibaki kwa sababu ilieleweka kwamba shughuli za Bunge ni za Wabunge. Hakuna Mbunge hata mmoja alitimuliwa. Ni nini sasa imetokea? Nchi yetu inarudi tulikotoka. Wakati ambao KANU ilikuwa inatawala, kwa mfano, ikitaka kuwakomesha Wabunge waliokuwa wakipinga Serikali wakati huo; askari walikuwa wanaletwa hapa, wanapewa mavazi ya Kimaasai na rungu. Waliwatwangwa Wabunge na kuwakimbiza mji mzima. Ilisemekana kwamba ni Wamaasai kutoka Narok wamekasirika kwa sababu Serikali ya KANU inapingwa. Bwana Spika wa Muda, ingekuwa namna hiyo na kama watu hawangepigana kubadilisha Katiba kwa lazima wakati huo, wewe, Bwana Spika wa Muda, unayekalia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}