GET /api/v0.1/hansard/entries/644961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644961,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644961/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, Kiswahili ni lugha ngumu kwa Sen. Elachi. Rais ni mgeni katika Bunge na hakuna Mbunge anastahili kuadhibiwa kwa kufanya kazi yake bungeni kwa sababu mgeni yuko pale. Ikiwa katika historia yetu, tunaanza mambo kama haya, basi, nchi hii inarudi nyuma katika mipango yake ya kidemokrasia. Rais alizungumzia mambo ya wanajeshi wetu walioko nchini Somalia. Kwanza, ninamuunga mkono Rais. Mipaka yetu, ulinzi wetu, imani na amani yetu lazima ilindwe kwa vyovyote. Tunastahili kuilinda nchi yetu. Mtu akituchokoza hapa, tunafaa kumfuata mpaka kwake kwa sababu tuna uwezo, nia na namna kama Wakenya. Lakini hata hayo yakiwepo,ukimfuata adui, humfuati hadi kwa nyumba yake na ukifika kwake unachukua kiti, kitanda chake, sufuria, familia yake na unakaa ndani ya ile nyumba. Hakuna vile utamueza yule adui ukikaa katika nyumba yake. Mtu akituchokoza, inastahili – tunajua makao ya Al Shabaab na wanakoishi – tunastahili kuwafuata mpaka pahali wanazalia lakini hatufai kwenda katika nchi yao. Kwa hivyo, Rais hakuwaambia Wakenya tumemfuata adui mpaka wapi na kwa nini wanajeshi wetu wanakaa katika taifa la Somalia. Hatuna biashara wala kazi ya kufanya Somalia. Kazi ni kulinda mipaka yetu. Kama hakuna amani na jeshi la kulinda amani linatakiwa kutumwa Somalia, hilo sio jukumu la Kenya. Hilo ni Jukumu la Umoja wa Mataifa. Wanafaa kuketi na kufanya hili na lile lakini sio kupeleka askari wetu na kuwajengea kambi ndani ya Somalia na kuwaacha pale. Wanavamiwa kama inzi, wanashikwa na kumenywamenywa kama mandazi na watu ambao wanajidai kwamba tuko ndani ya nchi yao. Kama Rais hawezi kulitoa jeshi letu katika nchi ya Somalia, hawafanyii Wakenya sawa sawa. Taarifa yake ya kusema kwamba tumedhibiti ulinzi wetu Somalia ni maneno tu. Hakuna mtoto wa ndani na wa mbele. Hakuna hata mmoja wa viongozi wa nchi hii ambaye amemtuma mtoto wake kwenda Somalia. Watoto wao wanalindwa, wanakula na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}