GET /api/v0.1/hansard/entries/644963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644963,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644963/?format=api",
    "text_counter": 271,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kukaa sawa sawa. Ni mtoto wa maskini anatumwa na umaskini wa mama na baba yake; ndio anaenda kumenywa kule na kuuawa na mambo yanaishia pale. Hata ridhaa ambayo Serikali ya Kenya inatoa haistahili hata kidogo ilhali mamilioni ya pesa inaibwa. Hatutavumilia na hatutaki mambo haya. Bw. Spika wa Muda, Rais alitoa ahadi na kusema kuwa Serikali yake imetimiza ahadi zote kwa miaka mitatu. Nataka kumkumbusha Rais akiwa pahali yuko kupitia mazungumzo yangu kwamba aliahidi watoto wetu wa shule za msingi vipakatalishi. Katika Bajeti ya mwaka wa kwanza wa uongozi wake, Rais alitenga Kshs26 bilioni ya kutoa vipakatalishi. Sisi sote tuliochaguliwa na hata wale ambao waliteuliwa katika Bunge hili wanaweza kuwa mashahidi wangu nikisema kwamba hakuna shule hata moja imepata vipakatalishi. Ikiwa mambo ya vipakatilishi haijatimizwa, inakuwaje Serikali inasema kwamba imeweza kutimiza ahadi zake zote baada ya miaka mitatu? Hayo ni maneno ya kufurahisha na hayana msingi na ukweli. Kwa wakati huu, Wakenya wanastahili kuambiwa ukweli na sio mambo ambayo hayafai. Bw. Spika wa Muda, tulisema na nimesikia watu wakizungumza hapa mambo ya rushwa na mambo mengine yanayoendelea. Kuna mtu alimkashifu Mbunge fulani kwenye mtandao. Ilimchukua siku nne kuandikisha mashtaka yake na kuenda kortini. Kwa sababu mtu huyo ni maskini, alitozwa faini ya Kshs5 milioni baada ya siku nne. Kuna mamilioni na mabilioni ya pesa zilizoibwa katika taifa letu. Ni taarifa tu tunasoma, kusikia au kuambiwa kwamba Serikali imejitoa mhanga kuhakikisha kwamba wezi wanaandamwa. Hakuna kaunti ambayo haijaathirika na wizi wa pesa katika kaunti zote 47. Mambo haya yote yako wazi. Hakuna jambo hata moja la kuficha. Hata hivyo, utapata kuwa gavana anachukuliwa saa nne na kutolewa kwa dhamana na saa sita au saa nane. Rais alituambia kuwa kuna kesi 300 za rushwa. Utapata kuwa mwizi wa mbuzi, vijiko, mandazi na mipira ya kunyonyeshea watoto maziwa anapelekwa kortini asubuhi na saa kumi na moja utasikia amehukumikwa kifungo cha miaka mitatu, mine au mitano. Katika kipindi cha uongozi wa hayati Mzee Jomo Kenyatta, wizi ulikuwa katika Serikali. Ulikuwa wizi usio wa mabavu wala si wizi katika benki. Katika Serikali ya Rais mstaafu Mhe. Moi, wizi ulianza kupenya na kuingia katika mashirika ya kibinafsi. Hivi leo, ni wazi kwamba hata Rais mwenyewe alisafiri kwenda Israeli na kuonyesha kuwa amebeba mzigo wa wizi mabegani ambao umemchosha. Alisema kuwa; Jamani Wakenya nawaomba tafadhali, mbona mmekuwa na maarifa ya wizi namna hii? Bw. Spika wa Muda, naomba uniongeze dakika mbili tu."
}