GET /api/v0.1/hansard/entries/644967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 644967,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/644967/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Leo tunasherehekea uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Kabla sijaketi, nataka kutoa ombi langu la mwisho katika taifa hili. Ninasema kama mwanachama wa Mrengo wa Coalition for Reforms and Democracy (CORD) ambaye nilikubali shingo upande uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Ninatangaza hapa leo kwamba labda mambo yangekuwa mengine ikiwa kesi haingepelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Viongozi wa Afrika wanaoongoza serikali za sasa wasifanye mapenzi yao kwa kujaribu kutoa taifa letu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa sababu inazuia mambo mengi. Aidha, inawafaya watu kuamini kwamba isipokuwa korti za hapa kwetu ni zile tunajua ni za wale ambao tumeona wakipelekwa kortini, kule nje kuna korti ambayo inaweza kuangalia maslahi ya wananchi. Naomba wenzangu kuwa tusijiondoe katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ili tuwe na sehemu nyingine ambayo inaweza kutisha wale ambao wanapanga kufanya makosa. Bw. Spika wa Muda, nashukuru."
}