GET /api/v0.1/hansard/entries/645043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645043/?format=api",
"text_counter": 66,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuomba mwongozo kutoka kwako. Alhamisi tarehe 31 Aprili, 2016, kulikuwa na maandamano yaliyofanyika ndani ya Bunge hili. Kwa masikitiko makubwa, miongoni mwa walioandamana ni mwanachama wa Kamati ya Spika. Bunge kama taasisi ina mila, desturi na kanuni. Nasikitika nikiuliza swala hili kwa sababu watoto wetu siku za usoni watakuwa Wabunge pia. Je, ni sawa kwa mwanachama wa Kamati ya Spika kuongoza maandamano ndani ya Bunge? Kama si sawa, hatua gani inayostahili kuchukuliwa kwa mwanachama wa Kamati ya Spika aliyeongoza maandamo ndani ya Bunge? Kama ni sawa, je, atakapokaa hapo unapokaa, ni sawa mimi nije na firimbi nimpigie?"
}