GET /api/v0.1/hansard/entries/645312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645312,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645312/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Tukiangalia upande wa usalama, inafaa ifahamike kwamba chini ya Serikali ya Jubilee, usalama umeimarika. Serikali ya Jubilee, kupitia kwa Wizara ya Usalama na Undani, imeweza kudhibiti ugaidi kwa kiwango kikubwa sana. Yafaa ifahamike kwamba ugaidi ni vita vya kidunia si vya Kenya peke yake. Kwa upande wa usalama, tumeweza kuona magari ambayo idara za usalama na polisi zimepatiwa. Ninaamini tuko na nguvu za kuwafukuza na kuwakamata magaidi na wataisha. Lakini, tisho kubwa la usalama nchini ni baadhi ya matamshi kutoka kwa viongozi wa kisiasa haswa wakiongozwa na vinara wa Upinzani. Upinzani sharti uwe lakini uwe na mwelekeo. Si Upinzani hohehahe. Wakiamka asubuhi ni matamshi mabaya yakupiganisha kabila tofauti, matusi na kusuta Serikali yao. Tunapokaribia uchaguzi wa 2017, tumesikia matamshi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Upinzani haswa rafiki wetu ambaye anafahamika kama baba, lakini ni babu. Tumeyasikia yale ambayo amesema kwamba asiposhinda, hili and lile litafanyika. Ameanza kutia Wakenya kasumba kwamba ni sharti ashinde. Usalama wa nchi hii unaanzia na mimi na wewe. Nikichangia kuhusu ufisadi, sijasikia Serikali nyingine ambayo imeweza kupiga kalamu maafisa wa kitengo cha juu kama Mawaziri. Hii ndio Serikali ya kwanza nchini kufanya hivyo. Kwa hivyo, vita dhidi ya ufisadi vinaanza na mimi na wewe. Nawashauri Wabunge wenzangu wanaohusika na maswala ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge wakomeshe ufisadi. Mhe. Rais alizungumiza kuhusu pesa za ugatuzi. Ni lazima tuelewe kwamba ugatuzi unakuja na changa moto zake na ni lazima ukweli usemwe."
}