GET /api/v0.1/hansard/entries/645346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645346,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645346/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninampongeza Rais kwa Hotuba yake iliyokuwa na mwelekeo katika uongozi bora wa nchi yetu. Sisi sote tuko hapa kuwawakilisha wananchi wetu. Ninampongeza kwa sababu Hotuba hii ilizungumzia mambo muhimu katika maisha ya mwananchi kule nyanjani. Kuna watu wachache ambao wanasema barabara hazijaenea. Ningependa kuzungumzia upande wa Kwale. Hata hivi tunavyozungumza, barabara ya Lunga Lunga kuanzia Msambweni inarekebishwa. Barabara hii ilizungumziwa na Rais. Kuna zabuni ambazo ziko tayari na mwezi ujao Rais mwenyewe anaenda kuanzisha mradi wetu wa barabara ya Kinango kuelekea Lunga Lunga ambayo itawekwa lami. Kwa hivyo, upande wa barabara, tunaweza kusema kuwa serikali inatengeneza barabara ili wananchi wawe na usafiri mzuri. Kuhusu mambo ya hospitali, Rais wetu ametuonyesha kupitia serikali yake kwamba ametafuta pesa kupitia Bunge hili na tukapata vifaa ambavyo vimeanza kuwekwa katika hospitali zetu ili kusimamia matibabu ya wagonjwa mahututi, matibabu ya saratani na magonjwa mengine. Kitu cha kusikitisha ni kwamba mashini hizo hazijafikishwa katika serikali za kaunti, hasa Kwale. Mashini zetu hazijafikishwa kwa sababu hakuna mahali pa kuziweka licha ya kwamba hospitali zenyewe ziko. Mashini hizi ni kubwa sana na zina uwezo mkubwa. Hospitali zetu hazina nafasi ilhali tumezipatia kaunti zetu pesa ili zitayarishe hospitali hizo ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi tukishirikiana na serikali kuu. Kwa upande wa elimu, Wizara ya Elimu imejaribu kwa sababu tumeona mpangilio mpya wa kubadilisha mfumo wa elimu wa 8-4-4 ili watoto wetu waweze kuwa na elimu ya kuwawezesha kutengeneza au kurekebisha vifaa kinyume na vile ilivyo sasa. Hata hizo mashini ambazo tumeletewa katika hospitali zetu, hatuna wataalamu ambao wanaweza kuzirekebisha zinapoharibika. Hii inatokana na elimu ambayo imekuwa ikipatiwa watoto wetu. Kwa hivyo kuna mpangilio mzuri ambao umeelekezwa katika hali ya matibabu. Kuhusu ajira kwa vijana, ni vyema ieleweke kwamba si lazima mtu aajiriwe katika afisi ya Serikali. Kupitia kwa mpangilio wa asilimia 30, tumeweza kuwaona vijana na kina mama wetu wakichukua zabuni na kuanza kufanya biashara. Hiyo ni njia moja ya kuongeza ajira katika mpangilio ule ambao ulikuwa umewekwa na Serikali. Ninataka ieleweke kwamba tumeanza mipangilio kupitia katiba mpya ya Kenya. Neno hili haliwezi kuwa asilimia 100. Linaenda kwa mipangilio. Kwa hivyo tuendelee kuiunga mkono Serikali na kama Wabunge, tusukume na kusimama kidete kupambana na ufisadi ili yale yote yaliyopangwa yatekelezwe kwa wakati unaofaa. Ninampongeza Rais kwa Hotuba yake na kazi nzuri anayoifanya."
}