GET /api/v0.1/hansard/entries/645373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645373,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645373/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "machache. Ninakubaliana na mwenzangu ambaye ameongea sasa hivi. Ni kweli kwamba lazima tujadiliane kuhusu mazungumzo ya Rais. Yale yamefanyika mazuri tuseme yamefanyika vizuri. Kama kuna shida, tujue ni sisi tunahitaji kama Bunge kuijadili. Ninashangaa sana kuona kwamba kuna watu ambao hawaoni kitu kizuri kwa Serikali hii. Ni mambo ya kushangaza sana. La pili, ningependa kusema kwamba sisi tuna Katiba ambayo tulipea Rais iliyotengenezwa na Wanjiku. Tulimpatia Rais na kumwambia kuwa tunataka afuate Katiba na mikakakati ambayo tumeweka kwa Katiba. Lakini nimeona wapinzani wetu wengine wametengeza Katiba nyingine ya mazishi ambayo wanataka tuitumie kufuta tume ya Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) na watu wote kazi. Hilo haliko kwa Katiba. Haiwezekani kwa sababu Rais anafuata Katiba ambayo tulimpatia. Hii Katiba ya mazishi inataka tufute IEBC na EACC. Hii Katiba inasema kwamba majaji si wazuri, polisi si wazuri mpaka bibi zao si wazuri. Where are we going in this country? We must respect the law ya kusema hii ni nzuri na hii si nzuri. Inafaa tufuate haki. Hatusemi watu wote wa CORD ni wabaya, hapana. Watu kama Mhe. Otuoma na wengine we respect them. They have been in the Government. Wanajua sheria na utaratibu wa kufanya mambo. Wakati tunaongea kuhusu ufisadi, ufisadi uko na tunakubali lakini tunataka tuulize, Uhuru Muigai Kenyatta alipoingia uongozini, alikuja na malaika kutoka mbinguni ama alikuta watu wale wale? Miaka yote wamekuwa hapa kwa ufisadi. Tunahitaji kujua. Hata Wabunge hakukuja nao kutoka mbinguni. Ni wale wale. Lakini hainistaajabishi kwa sababu ninajua kwamba kuna wale waliosema Yesu asulubiwe na mwizi aachiliwe. Ni kama hawa tu tulionao hapa duniani. Kwa hivyo, tusijali haya mambo ya kelele. Tufanye kazi ya haki inayotakikana. Nimesikia mwenzangu mmoja akisema hapa kwamba kuna kabila moja linaloajiriwa. Mambo haya si kweli. Hayo ni mambo ya uongo na hatutaongoza nchi hii na uongo ambao unawasilishwa kama ukweli. Uongo unaowasilishwa kama ukweli hautatusaidia katika nchi hii. Lazima tuzungumze ukweli kama viongozi. Tunaposema kabila moja ndilo linaloajiriwa si kweli. Sisi Wabunge tuliona kabila moja na ndugu wawili wanaotoka kaunti moja wakipiga firimbi. One tribe. It is on record . Ni kabila moja lilifanya haya mambo yote hapa. Out of 42tribes, kabila moja lilifanya haya mambo hapa. Hatuwezi kusema ni Wabunge wa CORD wote walifanya mambo hayo, lakini walifanya vibaya kwa kupiga firimbi na hata mimi nilishangaa. Kama unapiga firimbi kama Rais hajaongea, inaonyesha wazi kuwa ni mpango uliopangwa na ni vita vya kisiasa. Unahitaji kumusikiliza Rais akiongea kwa sababu tuna muda kama huu kuzungumzia aliyoyasema. Ni vibaya Rais akienda kusimama unapiga firimbi. Wakati chama chenu kitachagua Rais na sisi tukiwa upande wa Jubilee tupige firimbi, itakuwaje? Hilo halitatupeleka mahali pazuri. Tunahitaji kuwa na heshima. Nimeona Wabunge wakijadili hapa mambo mengi ambayo yanawahusu. Wao wenyewe wanahitaji kutunga sheria hizo. Ukiangalia mambo ya ufisadi, utakuta inakumba pande zote mbili, na si upande mmoja. Mwizi ni mwizi. Akiwa Muluhya, akiwa Mukikuyu, akiwa Mujaluo au Mukisii, ni mwizi. Kwa hivyo tusichanganye na kusema ni sehemu moja tu ya Jubilee inayokumbwa na ufisadi. Mwisho, katika vituo vya redio, wabunge wengi wa CORD walisema jinsi Serikali hii ni mbovu lakini dakika ya mwisho walipoulizwa kama watachaguliwa, walisema “ndio”. Kwa nini: “Kwa sababu nimejenga barabara, nimejenga shule na nimeweka maji,” Umeweka na pesa za nani? Hizi ni pesa za Serikali ya Uhuru Muigai Kenyatta zinazokusanywa kama kodi. Usiifiche Serikali kwa kujipeleka mbele na ilihali wewe huna kodi unayokusanya. Ni utawala wa Jubilee The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}