GET /api/v0.1/hansard/entries/645403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645403/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ninazungumza kutoka ndani ya moyo wangu kwa sababu ni tukio lililotokea katika eneo bunge langu. Nyumba ya nyasi mara ya kwanza imepata umeme. Chongo haambiwi tazama. Kama huna macho ni bahati mbaya kwa sababu hata miwani haitakusaidia. Angalia maswala ya usalama. Alipopata hatamu ya uongozi babake Rais Uhuru Kenyatta alikuwa na changamoto tatu kubwa. Ya ujinga, ya umasikini na ya maradhi. Leo angefufuliwa Hayati Kenyatta na kutawala Kenya, atapata changamoto ya ufisadi na usalama. Matatizo ya ughaidi na usalama si matatizo yanayokumba taifa la Kenya pekee. Ni matatizo ambayo yanakumba ulimwengu wote. Inafaa mataifa yajumuike pamoja ili yaweze kushinda hawa maghaidi. Tunaambiwa kwamba inafaa majeshi yetu yaondolewe huko Somalia. Si sisi wa kwanza kupoteza wanajeshi Somalia. Marekani wamepoteza mamia ya wanajeshi wao huko na vile vile Burundi. Kulinda taifa ni lazima ujitolee. Si Rais Uhuru alipeleka wanajeshi Somalia. Ni tukio lililomtangulia yeye na anaunga mkono tu kama Rais wa taifa. Wakati mwingine ninasikitika. Wakati ICC ilipotupilia mbali kesi ya Mheshimiwa Ruto hivi juzi, Kiongozi na Kinara wa Upinzani alimuunga mkono Mheshimiwa Ruto. Jana usiku akiwa Ufaransa alisikitika ni kwa nini kesi ilitupiliwa mbali. Unafiki haupeleki Kenya mahali."
}