GET /api/v0.1/hansard/entries/645405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645405,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645405/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ukiwa ndani ya nchi unasema “Oooh nimefurahi kesi ya Mheshimiwa Ruto imetupiliwa mbali” lakini unapotoka nje ya Kenya unasema “Oooh nimesikitika kesi ya Mheshimiwa Ruto imetupiliwa mbali”. Kwani hatukuoni ukiwa huko? Kenya inataka kiongozi atakayesimama kwa ukweli, na kama ni mbaya ni mbaya na kama ni chema ni chema. Leo unamuunga mkono Mheshimiwa Ruto na kesho unamkashifu! Kabla sijamaliza, nimesikia wakulima wa kahawa wamesamehewa na hawatalipa madeni yao. Nilikuwa ninasikiliza kwamba deni la wakulima wa Bura limesamehewa. Ninafikiri Rais alisahau na ningependa kumukumbusha. Makabila si 42. Ninataka taifa lijue kwamba kuna kabila la Munyoya na Malakote."
}