GET /api/v0.1/hansard/entries/645424/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645424,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645424/?format=api",
"text_counter": 183,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "muda mrefu basi angetueleza. Angetupa kiwango cha siku watakazo kuwa kule. Kwa maoni yangu, naona kuwa tunahatarisha wanajeshi wetu kwa sababu wanapambana na adui wasiemjua. Wanajeshi wetu ni hodari, wana silaha, uwezo na mafunzo mazuri lakini shida ni kuwa hawajui adui wanaepambana naye. Ikiwa tutaendelea kuwaacha wanajeshi wetu Somalia basi wataendelea kupoteza maisha yao. Pendekezo letu ni kuwa Rais angesema kuwa wanajeshi wetu watoke huko tuje tulinde taifa na mipaka yetu kuhakikisha kuwa adui hatatuingilia tena. Ni sawa kwenda kwa mara ya kwanza, kwenda kuweka sawa nchi jirani lakini kwa sasa ni vyema warudi. Si vibaya kwa sababu hata Jeshi la Amerika walitoka walipovamiwa kwa sababu haijulikani adui tunayepambana naye. Rais hakuzungumzia suala hilo. Vilevile, hakuzungumzia jinsi familia za wale wanajeshi waliopoteza maisha yao zitachukuliwa. Hao ni vijana wadogo waliooa hivi juzi na wana watoto wadogo. Serikali ya Jubilee haijasema vipi itawasomesha watoto wao. Jambo hilo haliko wazi. Rais alizungumzia ardhi ambayo imekombolewa Pwani haswa sehemu ya Waitiki. Nakubaliana na Rais kuwa Serikali iliweka mazungumzo lakini kusema kuwa Serikali ya Jubilee imekomboa shamba la Waitiki sio ukweli. Wananchi ndio wamenunua shamba hilo kwa sababu iliwaelekeza kufanya hivyo. Si ukweli kusema kuwa Serikali imekomboa bali ilileta mazungumzo karibu na kuhakikisha kuwa jambo hilo linafanyika. Kuhusiana na Barabara ya Port Reitz haswa katika eneo la Mombasa, ni kweli kuwa kuna barabara inayojengwa lakini inafadhiliwa na Benki ya Dunia. Tunataka kujua mgao wa taifa umefanya barabara gani katika kaunti ya Mombasa na Pwani. Mambo mengi yanafanywa na Benki Kuu ya Dunia wala sio kwa fedha za Serikali. Ni ukweli jinsi Rais alivyosema kuwa mataa yamengara katika kaunti nyingi lakini hiyo ni kwa sababu ya mkataba wa Benki Kuu ya Dunia na serikali za kaunti na hata gharama zote zinalipwa na serikali za kaunti. Ahsante Sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}