GET /api/v0.1/hansard/entries/645466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645466/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Shukrani Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Nia, malengo hata madhumuni ya Hotuba ya Rais ilikuwa nzuri ingawa kuna upungufu fulani. Nimepiga nduru sana. Nikiunganisha maneno niliyotumia kupiga nduru, yanawezatoka Lunga Lunga hadi Nairobi. Ni nduru ya tatizo la maji, wanyama na mengineyo. Wakati huu, ukisikia wananchi wanashindania maji na wanyama, si sawasawa. Katika Hotuba ya Rais, hakutaja mambo ya maji. Kule kwangu eneo Bunge la Mwatate, hali ya maji ni mbaya mno. Wananchi wanashindania maji na wanyama. Watoto wa shule saa zingine kwenda shule ni taabu. Akina mama wanaumia pia. Vitabu takatifu, Bible na Quran, kuna sehemu imetaja kuwa yule ambaye anaweza kumpatia mwenzake maji basi atapata baraka. Tuangalie masuala ya wanyama. Hili limekuwa suala sugu. Katika Hotuba ya Rais hakutaja. Kuna hawa wanyama wanaoharibu mimea ya wananchi lakini bado hawajapatiwa fidia. Na ni jambo ambalo tumeliongea kwa muda mrefu. Mahali pakavu kama kule kwangu Mwatate, wakati tumeona mvua kidogo,mwananchi akipanda mimea yake, ikiliwa na wanyama inakuwa ni taabu kubwa. Vile vile, ukiangalia katika eneo hili la Kenya kuna mahali ambapo pamebaguliwa ambapo hakuna viwanda wala nini. Siku hizi kupata kazi, kama hauna mtu mkubwa katika shirika fulani, kuipata ni vigumu. Mahali kama Mwatate kwa kweli, Serikali ingefikiria kuweka vitu kama viwanda ama kitu fulani cha kuwezesha wananchi wapate mapato. Kwa sasa hivi kule Mwatate hakuna njia yoyote mwananchi anaweza kujisaidia kupata mapato. Ni taabu moja kwa moja."
}