GET /api/v0.1/hansard/entries/645467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 645467,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645467/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Kuhusu elimu, kuna vyuo vikuu ambavyo viko katika haya maeneo ambayo yaliachwa nyuma. Hawana mafunzo ya ziada kama vile miji mikubwa kama hapa Nairobi na Mombasa. Utakuta kwamba katika hii Bajeti hivi vyuo vikuu vimepatiwa hela kidogo. Inakuwa vigumu sana kwa wale ambao wanaviongoza kuvishughulikia. Hata vingine baada ya muda mfupi labda vitaporomoka. Ile Hotuba ya Rais ingekua ingezingatia masuala yote na kuangalia pembe zote za Kenya, maanake ni Rais wetu wa Jamhuri. Angeangalia masuala yote haswa ya maji. Mwenyezi mungu alimpa hewa binadamu halafu ya pili ni maji. Bila maji, maisha si sawasawa. Asante kwa kunipa fursa hii kuongea masuala mawili au matatu."
}