GET /api/v0.1/hansard/entries/645469/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 645469,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645469/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Sisi tunaunga mkono Hotuba ya Rais na tunamshukuru sana kwa kuwa ameeleza Wakenya kuhusu ile kazi amefanya kwa hii miaka mitatu. Ile tu ningependa kuchangia pia ni kumshukuru kwa mambo ya barabara. Kama kaunti yangu ya Samburu, tunashukuru kwa sababu kutoka Rumuruti hadi Maralal tumeona barabara imeanza kutengenezwa. Katika miaka 50 tumekuwa tukililia hiyo barabara na sasa hivi inaendelea. Tunahimiza Serikali iweke nguvu kazi iende haraka kwa sababu kazi inaenda polepole . Tunamshukuru pia Rais kwa mambo ya hospitali na mashini za kaunti kwa sababu tunajua magonjwa mengi yanaenea katika kaunti bila hayo magonjwa kujulikana ni yapi. Wakiwa na hizo mashini, hayo magonjwa yatajulikana sana. Tunamshukuru sana Rais kwa kuimarisha mambo ya usalama na kuweka amani nchini. Tunamshukuru kwa sababu wakati alipochukua uongozi, usalama ulikuwa katika hali mbaya sana katika nchi yetu. Kila mwananchi ameona harakati zake za kuleta amani katika nchi yetu. Serikali yake ya Jubilee imefanya mengi. Hakuna mtu aliyefikiria kuwa kutakuwa na usalama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}