GET /api/v0.1/hansard/entries/645470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 645470,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/645470/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "nchini. Tunashukuru kuwa masuala ya kutokuwa na usalama yamerudi chini na kuangaliwa. Sisi pia tunachangia katika Serikali yetu ya Jubilee. Rais anafuatilia sheria za Katiba ambayo wananchi walipitisha. Kile tunachukia ni vile wenzetu katika CORD walifanya wakati Rais wetu anafuatilia sheria za Katiba ya Kenya na kuja hapa kueleza wananchi kile kinatendeka nchini. Wenzetu walianza kupigia Rais firimbi. Tulichukulia mambo hayo kama mambo ya utoto. Viongozi hawatakiwi kufanya hivyo. Naomba wenzetu wafahamu kuwa sisi ni viongozi katika Bunge hii. Wananchi wametuchagua kuja hapa. Ikiwa wanaona kuwa kuna mambo Serikali ya Jubilee haifanyi, wangekaa chini na kusema nini hakifanyiki. Sio kuja hapa kama watoto wa darasa la kwanza na kupigia watu kelele za firimbi! Siku hiyo tulivumilia kama Wabunge wa Jubilee. Wakati mwingine hatutavumilia. Hata sisi tutakuja na firimbi zetu. Tunapaswa kuwaheshimu Wakenya wote ambao wametuchagua kuja katika Bunge hili. Tunamshukuru Rais kwa kazi anayofanya."
}