GET /api/v0.1/hansard/entries/646421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 646421,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/646421/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii nichangia Hotuba ya Rais. Kwanza, ninawapongeza wanajeshi wetu wa Kenya ambao wako Somalia wakifanya kazi na kuona kuwa nchi hiyo imetulia kama nchi yetu ya Kenya. Kabla ya kuchangia yale ambayo Rais alisema juzi, ningependa kurudi nyuma kidogo katika hotuba ambayo aliitoa mwaka jana akisema kuwa ataweka Kshs10 bilioni kuwalipa watu ambao walifanyiwa dhuluma za kihistoria. Ninakumbuka mwaka huo tulichangia Hotuba ya Rais na tukasema kuwa jambo hilo halitawezekana. Nilipata fursa ya kuzungumza na kusema kuwa badala ya kuweka Kshs10 bilioni kwa watu ambao wamedhulumiwa kihistoria, afadhali pesa hizo zingewekewa mabalozi wetu ambao wako kule mitaani wakifanya kazi ngumu. Mabalozi hawakupata kitu na pia wale waliopata dhuluma za kihistoria hawakupata kitu. Katika Hotuba yake, Rais amezungumzia kuhusu mradi mkubwa wa Standard Gauge Railway. Mradi huu unapita katika eneo langu la Miritini. Miradi hii lazima ije na faida. Faida kubwa inapaswa kumgusa yule mwananchi ambaye yuko pale chini. Katika eneo la Maganda ambapo mradi huo unapita, kuna mtu anaitwa Mzee Sombo ambaye mpaka sasa hajalipwa pesa zake. Pia, Salim Said katika eneo la Maganda hajalipwa pesa zake mpaka sasa. Watu ambao wanalipwa kutokana na mradi huu wanapigiwa hesabu ya nyumba lakini hawapigiwi hesabu ya ardhi. Kama ilivyozungumzwa na Rais, mradi huu utaleta faida lakini wakazi hawajaona faida yake katika makazi ambayo wananchi wanaishi. Watu hawa wamekuwa wakiishi pale wakijua kuwa kuja kwa mradi huu kutawasaidia. Kwa hivyo, tunataka tuangalie mambo kama haya. Serikali ya Kenya inapaswa kujua kuwa watu ambao walikuwa wanaishi pale miaka yote ni wananchi ambao lazima maslahi yao yaangaliwe ili waishi maisha mazuri zaidi kushinda yale ambayo walikuwa wanaishi mwanzo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}